Home » » BODABODA JIJINI ARUSHA WAAZIMIA KUFANYA MAANDAMANO‏

BODABODA JIJINI ARUSHA WAAZIMIA KUFANYA MAANDAMANO‏

 KATIBU WA UMOJA WA WAENDESHA  PIKIPIKI ARUSHA (UWAPA) Fabian Shayo  AKISISITIZA JAMBO WAKATI WA KIKAO HICHO

 BAADHI YA WANACHAMA WA UWAPA KIKAONI
MWENYEKITI UWAPA Godluck Rugemalira
Na Idd Uwesu Arusha yetu
Madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda jijini Arusha wameazimia kuandamana endapo jeshi la polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani litaendelea kuwakamata kwa kisingizio cha kukosa leseni kwa kuwa jeshi hilo limeshindwa kutoa mafunzo kama walivyokubaliana na viongozi wa umoja wa waendesha  Pikipiki jijini humo UWAPA
Wameyasema hayo kwenye mkutano wao uliokuwa na lengo la kujadili hali hiyo wakati kukiwa na makubaliano na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani ya kupewa mafunzo kabla ya kupatiwa leseni hizo
Katibu wa Umoja huo Fabian Shayo amesema kuwa mnamo tarehe 9 mwezi wa 6 mwaka huu Kamanda wa jeshi la polisi jijini hapa Liberatus Sabas aliitisha kikao na madereva hawa na kukubaliana kuwa watapewa mafunzo maalumu kabla ya kupewa leseni hizo, amesema hali hiyo inawashangaza sana na kuwa wamefanya kikako hicho ili kupata maoni ya wanachama wao juu ya kuamua kufanya maandamano au la yenye lengo la kuwataka polisi kuacha kamatakamata hiyo na kuachiwa wenzao waliokwishakamatwa.
Nao baadhi ya wanachama wamesema kuwa hali inawapa wakati mgumu wa kufanya kazi zao kwani wanakosa amani na kuwa mashaka hali inayopelekea wakati mwingine kupata ajali barabarani kwa kuwakimbia askari hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja huo Godluck Rugemalira amesema kuwa wao kama watoa huduma ya usafiri wana nia nzuri ya kuifanya kazi hiyo kwa kufuata sheria na kuongeza kuwa hivi sasa wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanakutana  viongozi hao wa jeshi la polisi ili kujua utaratibu wa mafunzo hayo kwamba yataanza lini na huku wao wakiendelea kuandikisha majina ya wanachama wao tayari kwa mafunzo na mwisho alitoa tamko rasmi kuhusu maandamano hayo
Hata hivyo juhudi za Blogu hii kumpata Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha zilishindikana baada ya kuwa safarini kikazi na hata tulipojaribu kumtafuta kwa simu haikupatikana.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa