Arusha
Home » » UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI

UHALIFU KWA MROMBOO WAPATA MUAROBAINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akisalimiana na waendesha boda boda, eneo la  kwa  kwamromboo waliohuduriia kwenye uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye  Kituo cha Polisi
  Baadhi wa wananchi waliohudhuria kushuhudia   uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye  Kituo cha Polisi Muriet.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kushoto) akiweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Kituo cha Polisi Muriet.
 Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwa na wafadhili Mr. Haroun, Mrs Haroun pamoja na Sailesh Pandit baada ya uwekaji wa Jiwe la Msingi.
Mke wa Mfadhi  Mrs Haroun akivishwa vazi la Kimasai na wakazi wa eneo hilo kama shukrani yao kwa kujengewa Kituo cha Polisi.  


Nteghenjwa Hosseah, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ameweka Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi Kata ya Muriet wakati wa ziara ya Kikazi Jijini hapa yenye lengo la kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi.
Akiweka jiwe la Msingi Mhe. Gambo amesema kwa muda mrefu alikua anakerwa na uhalifu uliokithiri katika eneo hilo na hali hiyo kumsukuma yeye kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa kituo cha Polisi kitakachosaidia kudhibiti masuala ya Uhalifu.
Aliongeza kuwa baada ya kumpata mfadhili huyo alimlete eneo la ujenzi ambapo pia wahalifu walimuibia Simu yake mbele ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndipo na mfadhili alipopata ari ya kuanza ujenzi huu haraka iwezekanavyo.
“Haiwezekani mtu anaiba mbele ya Kamanda wa Polisi hakika hii ilituthibitishia kwamba uhalifu katika eneo hili umekithiri na kwa sababu hakunha Kituo cha Polisi wahalifu wanapata mwanya wa kufanya kazi hii isiyo halali kwa ujasiri zaidi” Alisema Gambo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mfadhili ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Lodhia Ndg. Haruni alisema amejitolea sehemu ya mali zake ili kuwasaidia Watanzania wenzake wanaoteseka na tabia za uhalifu zinazorudisha nyuma maendeleo
Ujenzi wa Kituo hicho utakaogharimu zaidia ya Tsh Mil 200 utakamilika mnamo mwezi Juni 2017.



 



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa