Arusha
Home » » Madiwani watakiwa kuhakiki majengo

Madiwani watakiwa kuhakiki majengo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WADAU wa maendeleo katika Jiji la Arusha na viunga vyake wameshauriwa kushirikiana na kujadili mpango kabambe wa maendeleo ya mpango mji badala ya kila mtu kuvutia upande wake.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, amewasihi madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Halmashauri ya Meru kuhakikisha majengo yote ya serikali na taasisi za umma yanapimwa ili kudhibiti wavamizi wa ardhi.
Ntibenda aliyasema hayo jana jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na madiwani wa Halmashauri zote tatu ambao baadhi yao ni wapya walikuwa wakipewa mafunzo kwa ajili ya mpango kabambe wa Jiji la mji Arusha uwe wa kisasa.
Alisema mpango huo umelenga kuboresha Jiji la Arusha na serikali imetumia zaidi ya Sh bilioni nane kwa ajili ya kuhakikisha majiji ya Arusha na Mwanza yanapangwa vizuri .
Alisema ni vyema madiwani hao ambao baadhi yao ni wapya kuhakikisha wanaojua mpango huo pamoja na kuupitisha kwenye Baraza la Madiwani ili uweze kupitishwa na kuanza kazi Julai. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, aliomba madiwani wa halmashauri zote tatu kuhakikisha wanasimamia maazimio ya Baraza la Madiwani ili kusimamia mpango huo.
Mwenyekiti wa Mipango Miji wa Jiji la Arusha, Diwani wa Moshono, Paulo Matsei, aliwataka wanasiasa kuacha siasa badala yake wasimamie sheria kudhibiti wanaoharibu maendeleo.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilisaini mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Subrana International Pty Ltd ya nchini Singapore kwa ajili ya kuendeleza majiji ya Arusha na Mwanza pamoja na viunga vyake.
Makubaliano hayo zilisainiwa mwaka juzi jijini Arusha na mkataba huo wa makubaliano unatakiwa ukamilike Julai 2016 huku kazi kubwa ikiwa ni kupanga Mji wa Arusha kuwa wa kisasa zaidi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa