Arusha
Home » » KESI YA UBUNGE LONGIDO: Shahidi adai mfumo wa kompyuta ulikosea hesabu

KESI YA UBUNGE LONGIDO: Shahidi adai mfumo wa kompyuta ulikosea hesabu

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Zhakaria ni shahidi wa 10 wa kesi ya uchaguzi Jimbo la Longido mkoani Arusha, alitoa ushahidi wake mahakamani mjini hapa mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, Silvangirwa Mwangesi.

Mtaalamu huyo wa kompyuta ambaye inadaiwa ndiye aliyekuwa akiingiza kura za fomu 21b za vituo vyote 175 katika jimbo hilo kwenye kompyuta kuu ya tume, alisema hayo wakati akihojiwa na Wakili Edmung Ngemela mbele ya Jaji Mwangesi.

Alidai mfumo mkuu wa Tume ya Uchaguzi wa uingiza kura kutoka katika vituo 175 vya jimbo la Longido uliposhindwa kufanya kazi kila kitu kilikuwa ni matatizo. Shahidi huyo alidai waliamua kurudia kuhesabu zaidi ya mara tatu lakini matatizo hayakumalizika.
Alidai hata hesabu ya mwisho iliyomtangaza mgombea wa Chadema, Onesmo ole Nangole kuwa mshindi ulikuwa na matatizo na kasoro za kimahesabu.

Pia shahidi huyo alikiri mahakamani hapo kuwa hata hesabu zilizokuwa katika kiapo chake zinatofautiana na zilizotangazwa na kumpa ushindi Nangole kwani kasoro za kimahesabu zilikuwa nyingi na zilitofautiana.

Shahidi wa 11 Sinyak Merita (48) ambaye alikuwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kamwanga wilayani Longido mkoani Arusha yeye alidai hakukuwa na malalamiko ya raia kutoka nchi jirani ya Kenya kwamba walikwenda kupiga kura katika kata yake kuanzia kujiandikisha hadi uchaguzi.

Alidai hakukuwa na malalamiko yoyote juu ya kuwepo kwa Wakenya katika kata hiyo na kama kuna shahidi alisema walikuwepo yeye hakuwa anawajua. Merita alikiri kutowakagua watu waliokuwa wamejiandikisha katika daftari la kupiga kura kwani aliamini kuwa waliojiandikisha wote walikuwa raia wa Tanzania na wenye miaka zaidi ya 18.

Shahidi wa 12 ,Tito Mndeme {51} msimamizi kata ya Kimokowa yeye alisema kuwa alisimamia vituo 11 vya kata hiyo na alihusika kubandika majina ya watu waliojiandikisha katika vituo vyote.

Mndeme ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi kwa miaka 27 alisema kuwa alihusika kusimamia uandikishaji lakini hakusikia malalamiko kama kulikuwa na watu raia kutoka nchi jirani ya Kenya walijiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka jana.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Longido ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, Felix Kimario anatarajiwa kutoa ushahidi wake leo na kufunga ushahidi wa upande wa mjibu maombi. Mwanasheria wa Serikali, David Akway alimweza Jaji Mwangesi kuwa Mkurugenzi atakuwa shahidi wao wa mwisho hivyo watakuwa wamefunga ushahidi wao .
Chanzo Gazei la Habari Leo
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa