Arusha
Home » » WAZIRI MKUU KASIMU MAJALIWA KESHO ANATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA KULINDA URITHI WA DUNIA NA AFRIKA JIJINI ARUSHA

WAZIRI MKUU KASIMU MAJALIWA KESHO ANATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA KULINDA URITHI WA DUNIA NA AFRIKA JIJINI ARUSHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri mkuu wa Juamuhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa akiwa anasalimiana na baadhi ya viongozi mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege cha kia tayari kwa ajili ya kufungua mkutano huo

Na Woinde Shizza,Arusha

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa kesho  anatarajiwa kufungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu  utakao fanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha unaotarajiwa kufanyika kwa siku nne .

Akiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi wakati akiongea na waandishi wa habari jijini hapa juu ya maandalizi ya mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa serekali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na shirika la UNESCO  nakituo chake cha urithi wa dunia.

Alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo yanatishia  na kuadhiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika afrika .

Aidha mkutano huo utapendekeza suluisho kwa kupitia upya shughuli zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.
Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea kwenye maeneo urithi wa dunia  kutokana na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.

Aliongeza kuwa pia  mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO  ya mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa uridhi wa dunia.

“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia uatakuwa na manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageniwatakao uthudhuria  mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na kujenga mataji wa kijamii”alisema Malinzi

Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa