Arusha
Home » » KESSY: WABUNGE WAPENDA RUNINGA NENDENI SALUNI

KESSY: WABUNGE WAPENDA RUNINGA NENDENI SALUNI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa ananyesha baadhi ya kadi za chadema ambazo zilirudishwa katika mkutano huo wa adhara


 Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Taifa Ndg SHAKA HAMDU SHAKA awataka viongozi wa jumuiya kujifunza KUTOKA wilaya za SAME na SIMANJIRO kwa ufanisi na ubunifu wa kuongoza Jumuiya

Na Woinde Shizza,Kilimanjaro

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Same Mkoa Kilimanjaro Augostino Kessy amewataka wananchi wapenda amani na maendeleo ya kweli kuwapuuza wabunge wa upinzani waliokwenda bungeni badala ya kuwawakikisha wananchi  wameamua ili waonekane kwenye runinga .

Amesema aina ya wabunge hao wameshindwa aidha kujua majukumu yao ya kuwepo kwao bungeni au wanataka waonekane kwenye TV bila kujali gharama zinazopunguza kujehgeka kwa ustawi wa uchumi wa wananchi hasa wanaoishi vijijini.

Kessy alitoa matamshi hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya stendi ya mabasi Same Mjini mkoani humo.

Alisema ni aibu na fedheha mpya kusikia wabunge ambao wamepewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wakikataa kushiriki vikao vya bunge hadi waonekane kwenye runinga.

"Huu ni upuuzi wa kisiass na utoto wa mwisho wanaoufanya wabunge wa upinzani, kama hawajui dhamana walionayo wakajifunze ccm, kama wanataka ubishoo basi  waende saluni "alisema

Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM  wilaya Same alisema vyama vya upinzani licha ya kukosa sera, dira na mipango vyama hivyo baadhi ya viongozi na wabunge wake hawana busara na si wazalendo.

Mapema Kaimu Katibu wa UVCCM wilaya same Neema Msangi alisema anaamini vijana wote waliosukunwa na upepo  yabis na kuhamia vyama vya upinzani bado wana nafasi ya kurejea na kupokelewa kwa heshima.

 Neema alisema viongozi wa upinzani ikiwemo ule umoja bwa ukawa hawakuwa na  mipango wala uwezo kuongoza Taifa ila walichokuwa wakikitafuta ni tsmaa ya madaraka,umaarufu na uroho wa fedha.

Hata hivyo katika hali ambayo haikutazamiwa na wananchi wengi wakaazi wa mji mdogo wa same ni mwanachama mfurukutwa wa chadema Amani Joseph Mgonja kukihama chama hicho na kujiunga na ccm.

Akizungumza katika mkutano huo mara baada ya kuchukua kadi ya ccm Mgonja alisema hakutaka chadema kwa bahati mbaya ila amekipima na kukichambua chama hicho na kukuta hakina malengo ya kujijenga kama taasisi ya kisiasa.

Kaimu katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka aliwabeza wanasiasa wa upinzani ambao wanapita huku wakisema anachofanya Dk John Magufuli ni kutekeleza ilani ya ukawa.

Alisems Dk Magufuli hakunadi ilani yenye sera za majimbo zenye lengo la kuigawa nchi kwa ukanda ,ukabila na uzawa ambayo alisema wananchi ikiwa wataingia kwenye mtego huo  wataitumbukiza shimoni na kuiletea majanga.

"Tumeishi kwa miaka 52 wote ni ndugu wa tumbo moja hakuna anayembagua mwenzake kwa rangi au kwa kabila lake, wanachotaka kukipandikiza chadema ni kulipasua Taifa".

Jumla ya wanachama 132 wa uvccm,ccm ,  chipukizi wa ccm na UWT walipewa kadi mpya na shaka ambaye yuko wilayani same kwa ziara ya kutazama utekekezaji wa ilani ya uchaguzi na uhai wa uvccm.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa