Arusha
Home » » AICC yamkabidhi RC madawati 100

AICC yamkabidhi RC madawati 100

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

UONGOZI wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) umemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 8.
Uamuzi wa menejimenti ya AICC kutoa madawati hayo ni kumuunga mkono Rais John Magufuli ya kutaka kila mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari, kusoma katika shule wakiwa wamekaa katika madawati.
Akizungumza kwa niaba na menejimenti ya AICC, Ofisa Mwandamizi wa Itifaki na Mahusiano wa AICC, Catherine Kilinda alisema AICC kama shirika la umma limeguswa na watoto wa shule kukaa chini na ndio maana limeunga mkono jitihada za serikali na kuamua kutoa msaada huo.
“Sisi kama shirika la umma linalojiendesha kibiashara tunaona fahari kuitikia mwito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuhakikisha watoto wetu wa shule hawakai chini; na ndio maana leo hii tumekabidhi msaada huu, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuinua sekta ya elimu,” alieleza Catherine.
AICC ambayo inajihusisha na kutoa huduma za mikutano, upangishaji wa ofisi na nyumba na kutoa huduma za afya, imekuwa ikitumia sehemu ya faida katika kusaidia jamii hususani katika sekta ya elimu Ntibenda alisema kwamba msaada huo ni sehemu ya juhudi za serikali mkoani Arusha, kuwashirikisha wadau wa maendeleo ili kuhakikisha shule zote za mkoa huo, zinakua na madawati ya kutosha.
“Naishukuru sana AICC kupitia kwa Mkurugenzi wa Mwendeshaji, Elishilia Kaaya kwa kuitikia vema mwito wa serikali ya Mkoa wa kuomba wadau wasaidie kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa wetu,” alisema Mkuu wa Mkoa.
Alitoa mwito kwa wadau mbalimbali mkoani Arusha, wakiwemo wafanyakazi wa ofisi ya Mkoa wa Arusha, nao kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi anakaa katika dawati.
Chanzo Gazeti La Habari Leo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa