Arusha
Home » » Ahsanteni kwa kuhamia na mimi Chadema- Lowassa

Ahsanteni kwa kuhamia na mimi Chadema- Lowassa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


by mbuya Godfriend
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewataka watanzania kuwa na imani na Chadema kwa kuwa maeneo yanayoongozwa na chama chichokatika halmashauri na majimbo yana maendeleo tofauti na maeneo mengine.
kata ya Moita Bwawani ambapo pamoja na mambo mengine amewashukuru wananchi waliompigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
''Wanakuja Simanjiro, Kiteto, Ngorongoro, Longido hawatuwezi na wakitaka waje maeneo haya walinganishe na maeneo yao hawatuwezi, ninawashukuru sana kwa kuhama na mimi toka CCM kwenda Chadema''-Amesema Lowassa.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu amesema chama chao siyo chama cha upembuzi yakinifu na urasimu bali chama chao ni chama cha kufanya kazi kwa vitendo ambapo watahakikisha wanapeleka maji eneo la Moita Bwawani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Isack Joseph amewataka watendaji na wenyeviti wa vijiji kutokuruhusu wakandarasi kufanya kazi bila wao kupata barua na kujirishisha na miradi itakayotekelezwa na kuhakikisha wanaisimamia ili iwe na tija kwa wananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa