Arusha
Home » » Diwani pekee wa CCM Meru afa

Diwani pekee wa CCM Meru afa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha
DIWANI pekee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Meru mkoani Arusha, Naftari Mbise amekufa juzi baada ya kuanguka juu ya mti, alipokuwa anapunguza matawi ya mti nyumbani kwake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Langaeli Akyoo alisema diwani huyo wa Kata ya Ngarenanyuki, mara baada ya kuanguka, alichukuliwa kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Tengeru na kufa akiwa njiani.
“Tunaendelea na taratibu za mazishi na tunatarajia kumzika diwani wetu siku ya Jumamosi,” alisema Akyoo.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha jana kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kifo cha diwani huyo ni cha kawaida.
“Kifo hiki ni cha kawaida na hivyo, hatutarajii kufanya uchunguzi kwani hakuna utata katika kifo chake...tunatoa pole kwa wafiwa,” alisema Kamanda Sabas.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shabani Mdoe akizungumzia tukio la kifo hicho alisema chama kimepoteza diwani mahiri na alikuwa diwani pekee CCM katika eneo hilo.
“Chama kimepoteza diwani wa pekee ukweli tumesikitika sana kumpoteza diwani wetu, lakini hii ni mipango ya mungu tumepokea,” alieleza Mdoe.

Chanzo Gazeti la Habari leo


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa