Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATENDAJI
wakuu wa mashirika mawili makubwa ya Umoja wa Mataifa ya Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) na
Shirika la Kimataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) wametoa wito kwa dunia
kujipanga vyema kumaliza kabisa tatizo la ukeketaji (FGM) ifikapo
mwaka 2030.
Katika
kauli zao walizotoa katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na ofisi ya
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam watendaji
hao Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dk. BabatundeOsotimehin, na Mkurugenzi
Mtendaji wa UNCEF, Anthony Lake, wamesema ipo haja ya dunia kuadhimisha
siku hiyo kwa kulenga kuwa na kiwango sifuri katika vitendo vya
ukeketaji.
Mashirika
hayo ya Umoja wa Mataifa yamesema kwamba ukeketaji ni vitendo vya
kikatili vinavyowanyima wanawake haki yao ya msingi na kuwazuia kuchanua
inavyostahili kama wanawake.
Viongozi
hao wamesema kwamba vitendo vya ukeketaji vimesambaa duniani kote
kuanzia Afrika, Mashariki ya Kati ambako imekuwa kama vitu vya kawaida
vikiathiri pia familia katika nchi za Asia Australia, Ulaya, Amerika ya
Kaskazini na Kusini.
Wamesema
kwamba kama hatua zisipochukuliwa kutokomeza ukeketaji idadi ya mabinti
na wanawake wanaoweza kuingizwa katika mkumbo huo itakuwa inaongezeka
ikiwapeleka katika mzunguko ule ule wa kushamirisha ukeketaji na
kurejesha nyuma maendeleo ya wanawake na binadamu kwa ujumla kama
familia.
“
Ili kuhami utu wa mwanamke, tunahitaji kuchukua hatua sasa na
kuwajibika kama dunia kutokomeza ukeketaji. “ ilisema sehemu ya taarifa
ya viongozi hao kwa vyombo vya habari.
Septemba
mwaka jana katika mkutano wa kutengeneza mpango wa kimataifa wa
maendeleo endelevu, nchi 193 zilikubaliana kuhakikisha kwamba ukeketaji
unakuw aumetokomezwa ifikapo mwaka 2030.
Taarifa
hiyo imesema kwamba ili kufanikiwa wananchi wanatakiwa kushawishi
familia nyingi duniani hapa kuachana na tabia ya ukeketaji.
“Tunahitaji kufanyakazi na idadi kubwa ya wataalamu wa tiba katika
jamii zetu – wakiwemo waganga wa jadi na wataalamu wa kisasa wa
matibabu, tukiwashawishi wakatae kutoa huduma ya ukeketaji.” Ilisema
taarifa hiyo.
Aidha
taarifa hiyo hiyo imetaka wanawake waliofanyiwa ukeketaji kusaidiwa
huduma mbalimbali zikiwamo za kisaikolojia na nyingine zinazostahili ili
kuwapunguzia maumivu waliyoyapata na wanayoendelea kuyapata kutokana na
kukeketwa.
0 comments:
Post a Comment