Arusha
Home » » TANZANIA AGRICULTURAL ORGANISATION (TASO) YAPATA VIONGOZI WAPYA WA TAIFA

TANZANIA AGRICULTURAL ORGANISATION (TASO) YAPATA VIONGOZI WAPYA WA TAIFA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Moja ya vyama muhimu katika kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini Tanzania ni Tanzania Agricultural Organisation (TASO). Pamoja na majukumu mengine, TASO ndio wamiliki na wasimamiaji wamaonyesho ya nanenane Nchini Tanzania. Hadi sasa TASO ina viwanja vitano vya maonyesho ya nanenane kwenye kanda za Kaskazini-Arusha, kandayalati –Dodoma, Mashariki – Morogoro, NyandazaJuu –Mbeya na Kanda ya Kusini – Lindi. Mfumo wa utendaji wa TASO umeanzia kwenye Kata, Wilaya, Mkoa, Kanda naTaifa. 

Juhudi zinafanyika kuanzisha viwanja vya maonyesho kwenye kanda ya Magharibi na kanda ya ziwa katika muda mfupi ujao. Tanzania ikiwa inatumia si zaidi ya asilia 25% ya Aridhi inayofaa kulimwa, Kilimo kinabakia kuwa msingi muhimu wa kukuza uchumi na ajira Nchini Tanzania. Pia izingatiwe kuwa Tanzania ina jumla asilimia 46% ya aridhi yote ya Afrika Mashariki hivyo kuwa na fursa kubwa ya kukuza soko na kulisha nchin yingine za Afrika Mashariki na nje.
Jumamosi yaTarehe 14 Novemba 2015 mjini Dodoma, TASO ilifanya uchaguzi wa viongozi wa Taifa ambao wataongoza taasisi hii muhimu katika kukuza kilimo kwa miaka 5. Viongozi waliochaguliwa ni Engelbert Moyo – Mwenyekiti, SharifaAbebe – Makamu Mwenyekiti, Imani Kajula – Katibu Mkuu, Daudi Mwalusyamba – Katibu Mkuu Msaidizi na Michael Lupyana – Mweka Hazina.
Akizungumza baada ya kuchaguliw aMwenyekiti wa TASO Taifa Engelbert Moyo alisema ‘’ Huu ni mwanzo mpya wenye malengo ya kuchochea mchango wa kilimo katika Uchumi, Maisha ya Watanzania, weredi katika kilimo na ajira. Ni fursa adhimu kuwa na viongozi waTaifa wenye ujuzi katika fani mbalimbali; Kilimo, Biashara, Masoko naFedha. Naamini kuwa TASO itapiga hatua kubwa katika kuwa muda muhimu katika kutoa mchango katika sekta hii nyeti’’.
Nae Katibu Mkuu wa TASO Imani Kajula alisema ‘’ Kilimo ni sekta yenye kuajiri watanzania wengi, lakini imekuwa na changamoto nyingi, tunatambua kazi hii tuliyopewa ni adhimu na muhimu katika kuleta mabadiliko ya kukuza soko la mazao, ubunifu watechnojia rahisi za kilimo, upatikanaji wa habariza kilimo, uvuvi, ufugaji na masoko kwa wakulima na pia kuboresha maonyesho ya Nanenane kuwa jukwaa la kuchochea ukuaji wa kilimo na ajira’’.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa