Arusha
Home » » WADAU WA ELIMU JUU KUKUTANA JIJINI ARUSHA.‏

WADAU WA ELIMU JUU KUKUTANA JIJINI ARUSHA.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


JenikisaNdile – MAELEZO
10/09/2015. Dar es salaam.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeandaa Kongamano la siku mbili la Elimu ya Juu litakalofanyika jijini Arusha kwa lengo la kuwa na jukwaa la kubadilishana uzoefu na maarifa miongoni mwa wadau wa elimu nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Prof. Yunus Mgaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam .

Amesema Kongamano hilo litaenda sambamba na Maonesho ya shughuli mbalimbali zikiwemo za utoaji wa huduma, na maonesho ya bidhaa mbalimbali kuonyesha mafanikio ya elimu  yaliyopatikana nchini.
Amesema washiriki wa mkutano huo kutoka taasisi mbalimbali watapata fursa ya kuchangia miradi elimu kwa ili kuinua sekta hiyo hapa nchini.

“Tunatarajia kuweka mikakati itakayowezesha kuwa na ushirikiano madhubuti baina ya Taasisi za Elimu ya Juu na Sekta Binafsi ili kubaini fursa na changamoto zilizopo tukilenga kuchochea maendeleo na kukuza ajira kwa wahitimu wetu ”, Alisema Prof.Mgaya.
Amefafanua kuwa Kongamano hilo la siku mbili litafanyika mnamo tarehe 1 hadi 2 Oktoba2015 katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha likiongozwa na  Kauli Mbiu isemayo “Kujenga Uwezo kwa ajili ya uzalishaji na ushinda ni Kitaifa :Matarajio na changamoto kwa muongo ujao”.

 Wizara ya Elimu imeandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Baraza la Taifa la Elimuya Ufundi (NACTE) Kamati ya Makamu wa Vyuo Vikuu nchini (CVCPT) pamoja na wadau wa Elimu ya Juu  kutoka ndani na nje nchi, Watendaji wa Serikali, Sekta Binafsi, Wabia wa Maendeleo, Taasisi zisizo za Kiserikali, Vyama vya Kitaaluma, Wahadhiri, Chama cha WaajirinaWanasiasa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa