Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza
akinamama wakimuelezea kero ya maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero
hizo Jimboni Longido.
Wakinamama wilayani Longido wakiendelea kuteka maji kwa zamu baada ya
kumaliza kumueleza kero zao Bi. Samia Suluhu aliepita maeneo hayo.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa katika vazi la kimasai alilopewa kama zawadi na wanaMonduli. Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kampeni ya CCM taifa wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza Bi. Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Bi. Samia Suluhu akimnadi mgombea ujumbe wa Jimbo la Monduli, Bi. Namelok Sokoine (kushoto) kwenye mkutano wa hadhara
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia
Suluhu.[/caption]
Na Joachim Mushi, Longido
WANAWAKE wa Wilayani Longido wamemsimamisha mgombea Mwenza wa
urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu njiani akielekea
jukaani kuhutubia wananchi wakimlilia kuwatatulia kero ya maji katika
Kata ya Longido ambapo kila familia imekuwa ikipata huduma hiyo mara
moja kwa wiki hali ambayo wamesema haikidhi mahitaji.
Bi. Samia alilazimika kusimama eneo ambalo wanawake walikuwa wamefurika
wakichota maji kwa zamu huku kila familia ikipewa idadi ya ndoo kumi
mara moja kwa kila wiki kiwango ambacho akinamama wengi walisema
akikidhi mahitaji kwa familia zao.
Mgombea huyo wa CCM aliwahakikishia akinamama hao kuwa yeye kama
mwanamke anajua shida ya maji inavyowatesa akinamama katika familia
ikiwa huduma hiyo inapokuwa tatizo katika upatikanaji wake, hivyo
atalisimamia suala hilo. Alisema Serikali ya CCM itakapoingia madarakani
imetenga shilingi bilioni 13 kwa ajili ya kupeleka maji eneo la Longido
mradi ambao utamaliza kero ya maji eneo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Longido Bi. Suluhu alisema kwa
kuwawezesha wafugaji wa eneo hilo wamepanga kujenga mabwawa ya kuvuna na
kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya nyakati za ukame kwa baadhi ya
maeneo, ikiwa ni pamoja na kujenga majosho ya mifugo na kuwezesha madawa
ya mifugo kwa wafugaji ili kuwaendeleza.
"...Kazi hii tutaifanya ndani ya kipindi kifupi mara tu baada ya
kufanikiwa kurudi madarakani, Serikali inayomaliza muda wake imefanya
mengi na sisi tutaendeleza na kuboresha zaidi. Alisema wanajua kilio cha
mahakama katika wilaya ya Longido hivyo mara baada ya kuingia
madarakani wataijenga.
Alisema akiwa njiani katika mikutano ya kampeni zake ameshuhudia uwepo
wa ukame katika vijiji lakini anawahakikishia hakuna mwananchi ambaye
atakufa na njaa endapo hali hiyo ya ukame itaendelea, kwani serikali ya
CCM katika ghala la chakula ina akiba ya kutosha.
Mgombea huyo mwenza wa CCM pia alifanya mkutano wa hadhara katika Jimbo
Monduli aliwaomba wanaMonduli kumpigia kura ya ndio mgombea urais kwa
tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza ilani ya
chama hicho ambayo pia imejumuisha ujenzi wa barabara ya Sanya Juu hadi
Longido na Longido hadi Mto wa Mbu wilayani Longido.
Aliwaomba wanaMonduli kumchagua mgombea ubungw wa Jimbo la Monduli kwa
tiketi ya CCM, Bi. Namelok Sokoine kwani mgombea huyo anarekodi na
historia nzuri ya utendaji kama alivyokuwa babayake marehemu, Edward
Moringe Sokoine. Aliwaomba pia kuwachagua madiwani wa CCM ili waweze
kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu.
0 comments:
Post a Comment