Arusha
Home » » WATIA NIA CCM WAENDELEA NA ZIARA YA KUJITAMBULISHA KATIKA KATA MBALIMBALI JIMBO LA ARUSHA MJINI‏

WATIA NIA CCM WAENDELEA NA ZIARA YA KUJITAMBULISHA KATIKA KATA MBALIMBALI JIMBO LA ARUSHA MJINI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SAM_4061Mtia nia ya ubunge kwa CCM Philemon Mollel akizungumza katika mkutano wa kujinadi mbele ya wana CCM wa kata ya Sinoni jijini Arusha ili kuomba ridhaa yakuteuliwa na chama chake kuwania ubunge wa jimbo la Arusha katika uchaguzi wa mwezi Oktoba Mwaka huu.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4098Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele ya wanachama wa chama hicho katika kata ya Sakina jijini Arusha ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwamgombea wa ubunge jimbo la Arusha kupitia CCM.
SAM_4041Mtia nia ya ubunge kupitia CCM mwanasheria Victor Njau akimwaga sera zake mbele ya wana CCM wa kata ya Sinoni jijini Arusha ili kuomba ridhaa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu.
SAM_4116Wanachama na waasisi wa CCM wa kata ya Sakina jijini Arusha wakisikiliza kwa umakini sera zinazotolewana watia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha walipokua wakijinadi kwao ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chaa chao kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
SAM_4177Kada wa CCM Mosses Mwizarubi anayeomba ridhaa yakuteuliwa na chama chake kuwania ubunge wa jimbo la Arusha akisisitiza jambo katika mkutano wa kujinadi uliofanyika katika kata ya Ngarenaro jijini Arusha.
SAM_4059Mtia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kupitia CCM Hamis Migire akijieleza mbele ya wanachama wa CCM wa kata ya Sokon One jijini Arusha ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti hicho kupitia CCM.
SAM_4157Mmoja wa wanachama wa CCM wa kata ya Sakija jijini Arusha ambaye hakujulikana jina lake mara moja akipitia kwa umakini kipeperushi chenye maelezo binafsi na mikakati ya kazi za ubunge cha mtia nia ya ubunge wa chama hicho Mustafa Panju wakati wa mkutano wa kujinadi wa watia nia hao uliofanyika katika kata hiyo.
SAM_4140Team kanitangaze wakifuatilia hotuba za watia nia ya ubunge kupitia CCM katika kata ya Elerai jijiniArusha 
SAM_4175Hapa ni sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba mbalimbali za watiania nafasi ya Ubunge
SAM_4155Wananchi waliojitokeza kuwasikiliza watia nia Ubunge CCM katika kata ya Ngarenaro jijini Arusha
    

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa