Arusha
Home » » YAMOTO BAND KUTIKISA ARUSHA‏

YAMOTO BAND KUTIKISA ARUSHA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
mwandagooooooo

Bendi maarufu ya Yamoto yenye makazi yake jijini Dar es salaam inayoundwa na vijana wanne jumamosi Mei 30 inataraji kutumbuiza katika jiji la Arusha katika onyesho la Usiku wa wanawake maarufu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mratibu wa onyesho hilo,Faustine Mwandago alisema kuwa bendi hiyo inataraji kupamba onyesho hilo ambalo wahudhuriaji wote watavalia vazi jeupe.

Alisema kuwa onyesho hilo litasindikizwa na wanawake maarufu kam Vera Sidika na Miss Tanzania 2015,Lilian Kamazima ambapo watapata fursa ya kuongea na wahudhuriaji wa onyesho hilo na kubadilishana mawazo.

Mwandago,alisisitiza ya kwamba onyesho hilo halina uhusiano na harakati zozote za kisiasa nchini tofauti na  minong”ono iliyopo chini kwa chini kwa sasa na kudai kwamba linalenga kuwaburudisha wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake.

Alitaja ukumbi utakaofanyika onyesho hilo kuwa ni Triple A uliopo katikati ya jiji la Arusha na kuwataka wakazi wa jiji hilo kutokosa kuhudhuria.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa