Arusha
Home » » NI LEO: SHETTA,DULLY SYKES KUNOGESHA TAMASHA LA USIKU WA MARAFIKI WA LOWASA JIJINI ARUSHA‏

NI LEO: SHETTA,DULLY SYKES KUNOGESHA TAMASHA LA USIKU WA MARAFIKI WA LOWASA JIJINI ARUSHA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
pichaaaaa
Na Pamela Mollel wa jamiiblog
Wasanii wawili wa kizazi kipya nchini Nurdin Billal maarufu kama Shetta na Abdulwaheed Sykes” Dully Sykes” kesho jumamosi  wanataraji kunogesha katika onyesho la kundi la marafiki wa waziri mkuu mstaafu,Edward Lowasa lililopewa jina la “ Usiku wa marafiki wa Lowasa” .

Onyesho hilo limeandaliwa na kundi la marafiki hao wa Lowasaa chini ya umoja wao unaojulikana kama “4 U Movement” linataraji kufanyika katika ukumbi wa burudani wa Triple A uliopo jijini Arusha ambapo mbali na wasanii hao pia wasanii wengine wachanga wanataraji kulisindikiza .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mratibu wa onyesho hilo,Jonathan Kassano alisema kuwa lengo kuu ni kuwakutanisha marafiki wote wa kiongozi huyo anayetajwa kuwania mbio za urais mwaka huu kufahamiana, kubadilishana mawazo pamoja na kubalishana ujuzi .

Mratibu huyo alisema kuwa onyesho hilo litaenea katika mikoa mbalimbali nchini ambapo mnamo Mei 20 mwaka huu kuanzia majira ya saa 4;00 usiku litafanyika  pia katika mkoa wa Dodoma na kisha kuelekea jijini Mwanza kabla ya kusambaa kote nchini.

Alisema kuwa kufanyika kwa onyesho hilo katika mikoa mbalimbali nchini kutawapa fursa marafiki wa kiongozi huyo ambaye  pia ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha kutawapa fursa marafiki hao kukutana na kufahamiana pia.

    

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa