Arusha
Home » » WAKANDARASI WAASWA KUJENGA MAJENGO YA SERIKALI NA WANANCHI YALIYO CHINI YA KIWANGO.

WAKANDARASI WAASWA KUJENGA MAJENGO YA SERIKALI NA WANANCHI YALIYO CHINI YA KIWANGO.




 Veronica Mheta, Arusha

WAKANDARASI wameaswa kuacha tabia ya kujenga majengo ya serikali pamoja na wananchi chini ya viwango kwalengo la kupata faida kubwa na kuleta hasara kubwa katika nchi.

Aidha serikali inafanya kila linalowezekana ili kulipa madeni ya wakandarasi wazalendo ikiwemo kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kuwezesha wakandarasi kupata zabuni za ujenzi wa majengo makubwa zaidi yanayojengwa na wageni kutoka nchi za nje.

Kauli hiyo ilitolewa jana Jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Mussa Iyombe wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa nne wa mwaka wa Chama cha Makandarasi Wazalendo Tanzania (ACCT) unaofanyika kwa siku mbili .

Alisema si vyema wakandarasi kufanya kazi kwa kutaka faida kubwa na kupelekea hasara kwa wananchi pamoja na serikali kwani ufanyaji kazi kwa kulipua unashusha heshima katika fani hiyo sambamba na kuleta hasara kwa serikali kwani baadhi ya majengo yanajengwa chini ya viwango.

Pia alisema hivi sasa serikali imefanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu (BoT) kwaajili ya kuwasaidia wakandarasi waweze kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka serikalini itakayowasaidia kupata fedha na kujenga majengo makubwa zaidi badala ya wageni kutoka nje ya nchi kupata zabuni za kujenga majengo hayo huku wakandarasi wazalengo wakiambulia asilimia 40 tu ya ujenzi.

“Naomba msibabaike na faida kubwa na kuleta hasara kwa Taifa angalieni uzalendo lakini najua mnaidai serikali fedha nyingi ila tuko mbioni kuwalipa madeni yenu na pia hivi sasa serikali itatoa mikopo yenye unafuu ili muweze kujenga majengo makubwa ya kisasa badala ya wageni kujenga maana wakipata faida wanarudisha kwao huku wakandarasi wazalendo wakiambulia kazi za matengenezo madogo madogo”.

Naye Mwenyekiti wa ACCT, Mhandisi Milton Nyerere alisema kuwa chama hicho kipo katika hatua ya kuanzisha chuo cha ufundi kwaajili ya kukuza uwezo kwa kuendesha mafunzo ya fani mbalimbali za kikandarasi kwa mafundi wa makampuni ya makandarasi ili kupunguza changamoto ya wataalam wanayokumbana nayo kwenye utekelezaji wa miradi.

Aliongeza kuwa chama hicho kinajumla ya wanachama 78 na kimekuwa na mahusiano mazuri na Bodi ya Wakandarasi (CRB)na wadau mbalimbali katika uimarishaji wa ubora wa kazi sambamba na kuanzisha taasisi ya fedha benki kwaajili ya makandarasi wazalendo ili kuwasaidia kupambana na changamoto ya mitaji.

Chanzo Michuzi Blog


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa