Arusha
Home » » SEREKALI YATAKIWA KUTOWAFUKUZA WATOTO WA KIKE WENYE UJAUZITO MASHULENI

SEREKALI YATAKIWA KUTOWAFUKUZA WATOTO WA KIKE WENYE UJAUZITO MASHULENI


Na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha
Serikali imetakiwa kutazama upya uwezekano wa kubadili sheria inayomnyima haki ya kuendelea na masomo mwanafunzi wa kike pindi anapopata ujauzito akiwa shuleni.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Afisa elimu taaluma ,mkoa wa Arusha,Kabesi katundu Kabeja wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa umoja wa wakuu wa shule za msingi kutoka nchi ya Kenya uliofanyika katika hotel ya Leons iliyopo Sakina kwa Idi ,jijini hapa,ambapo walimu zaidi ya 1000 kutoka nchini humo walikutana.

Alisema hatua ya sasa ya kumfukuza shule mwanafunzi wa kike mwenye ujauzito ni kumnyanyapaa na kumkosesha fursa ya kupata elimu,hivyo alisema ni vema serikali katazama upya sheria hiyo kandamizi.

Aliitaka serikali kuiga nchi jirani ya kenya ambayo sheria yao inaruhusu msichana huyo kuendelea na masomo pindi anapokuwa amejifungua.

‘’Hapa kwetu sheria zinakataza mwanafunzi mwenye ujauzito kuendelea na masomo lakini serikali tumeiomba serikali ibadili sheria hiyo ili kutoa fursa kwa mwanafunzi mwenye ujauzito kuendelea na masomo pindi anapojifungua,alisema Kabeja.

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja kutoka nchini Kenya ,Wintred Mbinyasila ,alisema mkutano huo ambao umekuwa ukifanyika kila mwaka unalenga kubadilishana mawazo na mwaka huu lengo ni kujifunza teknolojia ya kufundishia.

Hata hivyo alisema nchi ya Kenya imepiga hatua kubwa suala la elimu kwa mtoto wa kike baada ya kuruhusu mwanafunzi huyo pindi anapokuwa na ujauzito kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

‘’Serikali huchukua hatua kali kwa mtu mzima aliyempa ujauzito mtoto wa kike ila kama alipata ujauzito kutoka kwa mwanafunzi mwenzake ,sheria inaruhusu kuendelea na masomo kwa masharti ya kutoa matunzo pindi akifikia umri wa mtu mzima’’alisema

Naye mjumbe wa shirikisho la walimu wakuu wa nchi za Afrika mashariki ,Anjelina Kitigwa alisema mkutano huo unasaidia sana kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zilizopo hali itakayosaidia kuinua elimu katika nchi za afrika mashariki.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa