Arusha
Home » » KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA‏

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA‏

Ameongeza kuwa CCM ni chama kinachotakiwa kuwasemea na kuwatetea wanyonge na siyo kuwakandamiza na lazima viongozi na watendaji wa serikali na chama wawajibike kwa wananchi ambao ndiyo walioingia mkataba na CCM ambayo iliunda serikali inayotekeleza ilani yake .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Arusha akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali ya CCM na kuhimiza uhai wa Chama Cha Mapinduzi CCM akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ARUSHA)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchimba mfereji wa kupitisha mabomba ya maji katika mradi wa maji kata ya Olmot Olkaryan jijini Arusha. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kufungua maji ya bomba katika mradi wa maji kata ya Olmot Olkaryan jijini Arusha. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchimba mfereji wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Sombetini kwa Mromboo jijini Arusha. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Sombetini kwa Mrombo mara baada ya kukagua barabara hiyo jijini Arusha. 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali jijini Arusha. 8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua shina la wakereketwa la Sakina kwa Shamsi Arusha Raha jijini Arusha. 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kushoto akiongozana na Nape Nnauye na viongozi wa mkoa na wilaya ya Arusha wakati akielekea kutembelea soko la Kirombero jijini Arusha. 10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana wakati alipowasili katika soko la Kilombero jijini Arusha. 11Kada wa CCM Viola naye akimwaga maneno ya sumu wakati wa mkutano wa katibu Mkuu wa Ndugu Abdulrahman Kinana na wafanya biashara wa soko la Kilombero jijini Arusha. 13Nape Nnauye akizungumza na umati wa wafanyabiashara na baadhi ya wananchi mbele ya jengo la Soko la Kilombero jijini Arusha. 14Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wakiwa katika mkutano huo. 15Kiongozi wa wafanyabiashara wa soko la Kilombero jijini Arusha akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana huku Nape Nnauye akiwa amemshikia kipaza sauti. 10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili katika soko la Kilombero jijini Arusha. 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kata ya Remala Arusha kulia ni Diwani wa kata hiyo Bw.Karim Mushi. 18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Maendeleo Group Peter Samwel iliyotolewa na diwani wa kata ya Remala Bw. karim Mushi kulia. 19 Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Maendeleo Group Peter Samwel akijaribu kuendesha pikipiki mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pikipiki hiyo imetolewa kwa kikundi hicho na diwani wa kata ya Remala Bw. Karimu Mushi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa