Mkoa
wa arusha unaendelea kukabiliwa na ongezekao la uingizaji na utumiaji
wa vipodozi vyenye kemikali za sumu na vilivyopita muda wa matumizi
tatizo linaloendelea kutishia afya za wanawake na vijana kupata
magonjwa ya kansa ikiwemo ya ngozi.
Akizungumza baada ya mamala ya chakula na dawa kukamata tani mbili
za vipodozi vyenye viambata vya sumu na vilivyopita muda wa matumizi
katika maduka mbalimbali ya jiji la arusha afisa afya wa jiji hilo Bi. Anjela Mhitu amesema kama hali hiyo haitadhibitiwa na vijana na wanawake hawatawezeshwa kuepuka janga hilo wengi wataangamia. Meneja wa mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kaskazini Bw.Damas
Matiko amesema shehena ya vipodozi walivyokamata ina thamani ya milioni
saba na pamoja na jitihada wanazofanya tatizo bado ni kubwa na
amewaomba wadau wa sekta za afya kusaidia tatizo hilo kwa kudhibiti na
kutoa elimu ya madhara yanayoikabili jamii kama ikiendelea kutumia
bidhaa hizo. Mmoja wa watuhumiwa waliokutwa na bidhaa hizo amesema bidhaa
zilizokamatwa zilikuwa zimechanganywa ndani ya kontena la bidhaa halali
na amekamatwa wakati anazichambua ili akaziharibu maelezo ambayo hata
hivyo yamepingwa vikali na maafisa wa TFDA.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment