Arusha
Home » » LOWASSA ATAKA HAKI ZA MSINGI ZA WANANCHI KULINDWA

LOWASSA ATAKA HAKI ZA MSINGI ZA WANANCHI KULINDWA

MBUNGE wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameiomba Serikali kutokandamiza haki za msingi za wananchi kwa sababu ya haki za wanyamapori.
Akizungumza jana katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vitongoji huko Bwawani, Mto wa Mbu wilayani Monduli, Lowassa alisema pamoja na matatizo yaliyopo katika mipaka, lakini ni muhimu haki za raia zikalindwa.
“Hapa Bwawani najua mna matatizo na National Park. (Hifadhi ya Taifa) ...naomba Serikali isifanye haki za wanyamapori kwa kugandamiza haki za msingi za raia,” alisema Lowassa.
Aliongeza, “Tunaheshimu sana Utalii kwa sababu unatuingizia fedha, lakini tuheshimu haki za msingi za raia...na ninyi tuheshimu mipaka iliyowekwa.”
Eneo hilo limekuwa na mgogoro na Hifadhi ya Taifa ya Manyara inayopakana nayo, suala ambalo ni moja ya kero kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Akizungumzia wana CCM waliojitoa kutoka katika chama hicho Lowassa alisema; “anayetupinga, atupinge kwa hoja kama kero hazijatatuliwa...si unaamua kutoka halafu unataka uhongwe ili urudi.”
Aliongeza kuwa ndani ya chama wanagombania utekelezaji wa Ilani na hapo ni haki kwa mwanachama kukasirika iwapo Ilani haitekelezwi, lakini si vinginevyo, na kusisitiza kuwa mji wa Mto wa Mbu utabaki kuwa ngome ya CCM.
 Chanzo:habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa