Arusha
Home » » WANANCHI WAMTEGA DC ARUSHA

WANANCHI WAMTEGA DC ARUSHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela
WANANCHI  wa Kata za Mlangarini na Moshono, wamemuweka kiti moto Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela wakitaka awape jibu ni lini hasa watalipwa fidia ya maeneo yao waliyoyatoa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, (JWTZ) kikosi cha 977 vinginevyo wataanza kuyaendeleza kwa kujenga na
kulima

Aidha, wamedai Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliwaahidi wangelipwa fedha hizo mwaka 2012, lakini mpaka sasa hawajalipwa, hali inayowafanya waishi katika mazingira magumu.
Akisoma risala kwa niaba ya wenzake, Masamaki Mollel, alisema wanasikitika kuona maagizo ya Mkuu wa Mkoa yakishindwa kutekelezeka, kwani mbali na suala la fidia, pia agiza mawe na vibao vya mipaka vilivyokuwa vimewekwa awali na jeshi kwenye maeneo yaliyorejeshwa kwa wananchi viondolewe, lakini mpaka sasa vipo.
“Mkuu wa wilaya (DC) athari zinazotukumba kwa sasa ni kwamba nyumba zinatuangukia na haturuhusiwi kuzijenga wala kuzika katika maeneo haya. Uchumi wetu umedorora kwani hatuna vipato vingine tofauti na kilimo,” alisema Mollel.
Mwananchi mwingine, Isack Saikon, alisema mbali na serikali kuaihidi kuwalipa fidia tokea mwaka 2012, lakini mpaka sasa hawajaonyeshwa maeneo watakayohamia.
“Kwa maelezo yako mkuu wa wilaya unasema umefuatilia suala hili na sasa umechoka, sembuse sisi tunaoangukiwa na hizi nyumba …hatutaki ‘story we are fadeup’,” alisema Junice Mollel, mkazi wa Mlangarini,
Akijibu malalamiko  hayo, Mkuu wa wilaya, Mongela, alikiri suala hilo kuchukua muda mrefu, ila akawaomba wananchi kuvuta subira, kwani amezungumza na watu wa
Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Fedha wamemhakikishia fidia hiyo itatoka ndani ya wiki mbili zijazo.

“Ikifika  wiki mbili na hakuna dalili ya watu kutoka wizarani kuja kulipa fidia kama walivyotuahidi mimi na mkuu wa mkoa, nitakuja mwenyewe wala situmi mwakilishi, nitawaambia ile kauli sikudanganya ila naona wenzangu hawaji,” alisema Mongela.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa