Arusha
Home » » WAKULIMA 2,380 WAPEWA MBINU MPYA

WAKULIMA 2,380 WAPEWA MBINU MPYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WAKULIMA 2,379 kutoka Wilaya tano hapa nchini wamenufaika na elimu ya teknolojia mpya ya matumizi ya mbegu mpya za mahindi na mbaazi pamoja na kulima kwa kutumia kilimo mseto na kilimo hifadhi.
Mratibu wa mradi wa usalama wa chakula (Simlesa), kwa Tanzania, Mboi Mgendi, alisema awamu ya kwanza ya mradi huo ilianza mwaka 2010 na umeweza kuzinufaisha Wilaya za Karatu, Mbulu, Gairo, Kilosa na Mvomero.
Alisema kuwa lengo la mradi huo ambao umeishia 2013 ni kuwepo kwa usalama wa chakula kwa wakulima waliopo Wilaya hizo na kuondoa changamoto zilizokuwa zikiwakabili wakulima, ikiwemo ugonjwa wa mahindi
unaosababisha upotevu wa mazao.

Dk. Mgendi, alisema kuwa wafadhili wa mradi huo ni serikali ya Australia kupitia shirika la ACIAR, ambao walifanikiwa kuzifikia Wilaya hizo kutokana na elimu hiyo na kuongeza uzalishaji wa mazao hayo, ambako wakulima hao hapo awali walikuwa wakilima tani moja na kwa sasa tani mbili kwa heka.
Akizungumza katika mkutano unaozikutanisha nchi za Tanzania na Kenya jijini Arusha, Dk. Mgendi alisema  wanaangalia changamoto zilizokuwa katika awamu
ya kwanza ya mradi pamoja na mafanikio ili kuweza kuboresha awamu ya pili inayotarajiwa kuanza mwaka huu.

Alisema changamoto hizo ni wakulima kutokuwa na elimu ya kuacha masalia ya mazao shambani kama mradi unavyoelekeza ili kuweza kuzuia upotevu wa maji na kurudisha rutuba kwenye udongo.
Dk. Mgendi, alisema awamu ijayo watajaribu kupata mbegu kinzani zitakazovumilia magonjwa ya mazao, ili kuondoa changamoto ambayo imekuwa ikiwakabili wakulima mashambani.
Aliongeza kuwa mradi huo unatekelezwa katika nchi tano za Afrika ambazo ni Kenya, Tanzania, Malawi, Msumbiji na Ethiopia.
Chanzo Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa