Arusha
Home » » MKUTANO MKUU WA LAPF WAANZA ARUSHA

MKUTANO MKUU WA LAPF WAANZA ARUSHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MMKUTANO mkutano mkuu wa saba wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 700 kutoka ndani na nje ya nchi, umeanza jana jijini hapa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga, alisema maandalizi yote ya mkutano huo wa siku mbili wenye kauli mbiu ya ‘Maadhimisho ya Miaka 70 ya Ukuaji na Huduma Bora LAPF’, yamekamilika ambako utakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo.
Sanga alisema LAPF ndio mfuko unaoongoza si tu kwa kutoa mafao bora, bali pia kwa kuwa na afya bora, ambako kwa sasa una rasilimali zenye thamani ya sh bilioni 700. “LAPF pamoja na kuwa ndio mfuko unaolipa kwa haraka zaidi, ambapo mstafuu kama anastaafu kesho, LAPF wao wanalipa jana…ndio mfuko unaoongoza kwa utunzaji wa mahesabu kati ya mifuko yote kwa mujibu wa NBAA, na ndio mfuko unaokuwa kwa kasi zaidi kwa mujibu wa SSRA,” alisema Sanga.
Mkutano huo utafunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia na kufungwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka
chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa