Arusha
Home » » MAHAKAMA YAMFUTIA KESI NAIBU MEYA ARUSHA

MAHAKAMA YAMFUTIA KESI NAIBU MEYA ARUSHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe na Diwani wa levelos, Ephata Nanyaro
MAHAKAMA imeifutilia mbali kesi ya kumshambulia mgambo iliyokuwa ikiwakabili Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe na Diwani wa levelos, Ephata Nanyaro, (CHADEMA).
Uamuzi huo uliopokelewa kwa shangwe na viongozi hao na wafuasi wa CHADEMA, ulitolewa jana na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Chrisanta Chitanda, aliyekuwa akisikiliza shauri hilo la jinai namba 413/2014.
Alifikia uamuzi huo baada ya wakili wa Serikali, Mary Lucas, kueleza kuwa hati ya mashtaka bado haijafanyiwa marekebisho hivyo akaomba tarehe nyingine kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Hakimu Chatanda, alisema kuwa anatumia kifungu cha 125 cha uendeshaji wa shauri la jinai kufuta shauri hilo kutokana na upande wa Jamhuri kutoa sababu kila mara kwa lengo la kuchelewesha kuendelea kwa shauri hilo.
Awali wakati shauri hilo likiahirishwa mara ya mwisho Oktoba 7, mwaka huu Hakimu aliutahadharisha upande wa Jamhuri kuwa atalifuta shauri hilo endapo watafika mahakamani hapo na sababu ya aina yoyote kwa
ajili ya kuliahirisha.

“Tulipanga leo uwe usikilizwaji wa maelezo ya awali baada ya wakili wa serikali kusema upelelezi umekamilika, lakini leo wamekuja wanasema wanaomba muda wakafanyie marekebisho hati ya mashtaka nitaahirisha shauri hili kwa kipindi kifupi….
“Lakini wakirudi tena na vijisababu vyao vya kutaka shauri hili liahirishwe tena, nitalifuta,” alisema Hakimu Chitanda.
Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mnamo Aprili 16 mwaka huu wakiwa maeneo ya Levolos, Naibu Meya, Msofe na diwani Nanyaro wanadaiwa kumpiga mgambo William Mollel, kifuani na sehemu mbalimbali za mwili hivyo kumsababishia maumivu mwilini.
Wakizungumza mara baada ya uamuzi huo, Naibu Meya Msofe na diwani Nanyaro, walisema kuwa wameridhishwa na uamuzi wa mahakama kwa kuitupa kesi hiyo waliyodai kuwa ni ya kupikwa iliyolenga kuidanganya mahakama.
“Tunaamini siku zote katika haki na usawa, niwaahidi wananchi wa Arusha kuwa CHADEMA tutaendelea kupinga uonevu bila kujali vitisho, sisi tulipigwa na mgambo tulipoenda kuwaokoa wananchi waliokuwa wamenyang’anywa mali zao….
“Tuwahakikishie kuwa shauri hili limetutia nguvu zaidi na tuko imara kuwapigania wananchi, sisi ni watumishi wa wananchi ambao hatutayumba kuhakikisha wananchi wanapatiwa haki zao,” alisema Nanyaro.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa