Arusha
Home » , » KAMPUNI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI SAMSUNG YALENGA KUKUZA UCHUMI WA JIJI LA ARUSHA

KAMPUNI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI SAMSUNG YALENGA KUKUZA UCHUMI WA JIJI LA ARUSHA


Meneja Mkuu wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung Tanzania na Mr Nawaz Ladha Mkurugenzi wa  Kampuni ya Freedom Elektronics moja ya kati ya wasmbazaji wa  Samsung Tanzania akikata utepe kuzindua rasmi duka jipya na kituo cha huduma kwa wateja.
Meneja Mkuu wa Samsung Mr Mike Seo akiwahutubia wanahabari(hawapo kwenye picha) katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha.
Meneja wa Usambazaji wa Samsung akitoa maelezo kwa wateja na waandishi wa habari.
Meneja Mkuu wa Samsung Mr Mike Seo akiwahutubia wateja wa Samsung katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha.
Meneja  wa huduma Samsung Mr Mubarak Mikidad akiwahutubia wanahabari katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha.





Na Gadiola Emanuel -Arusha


Kampuni ya Samsung inazindua rasmi siku ya leo duka kubwa na kituo chake cha huduma kwa wateja lililopo barabara ya Sokoine mjini Arusha. Uzinduzi huo utawawezesha wateja wake wote mkoani Arusha kupata huduma stahiki na bidhaa halisi za Samsung. Kituo hiki ni cha kwanza kuzinduliwa mkoani Arusha na kampuni hii kubwa yenye idadi kubwa ya watumiaji na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni.
“Mtazamo wa maisha ya wateja hubadilika kwa kasi kubwa na kuwafanya kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma bora. Kama kampuni kubwa inayoongoza kuwa na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni, Samsung imefanya juhudi kubwa kuhakikisha inatimiza mahitaji ya wateja wake wote Afika. Mkoa wa Arusha hutegemea sana biashara kwani una wakaazi toka jamii mchanganyiko. Hivyo katika Afrika Mashariki, Arusha ni kitovu cha wageni toka nchi mbalimbali ulimwenguni. Kampuni ya Samsung ina imani kubwa kwamba kituo cha huduma kwa wateja kitatoa ushirikiano mzuri na kuboresha uhusiano kwa wateja wake mkoani Arusha. Kwasababu Arusha ni muhimu na kituo kikuu cha safari nchini Tanzania”, haya yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hii nchini Tanzania, Bw. Seo
Mbali na kuuza simu za mkononi na bidhaa za kielektroniki, duka hili jipya la Samsung litatoa huduma za ziada kwa wateja wake. Hii ni pamoja na kuwapa wateja wake watakaojisajili na uduma ya e-warranty usaidizi wa kiufundi bila malipo kwa kipindi cha miaka miwili.
Mpango huu utawanufaisha wateja wa Samsung kwa kusajili bidhaa zao kupitia Simu. Huu ni mchakato utakaofanyika kwa kutuma namba IMEI kwenda 15685. Baada ya kufanya hivyo wateja watanufaika na msaada wa kifundi kwa kipindi cha miaka miwili sambamba na kujipatia nafasi ya kushinda bidhaa mbalimbali za Samsung.
Katika kusherehekea uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinawasogezea wateja wake huduma karibu, kampuni hii kubwa duniani inawaletea habari njema wakaazi wa Arusha kwa kutoa punguzo kubwa la bei za bidhaa zake. Kwenye kipindi hiki cha ufunguzi bidhaa zitakazokuwa na punguzo la bei ni pamoja na; Luninga, feni, majokofu na vifaa vya nyumbani. Bila kuwasahau wateja wake wa simu, ambao watapewa wa bure vifurushi vya intaneti na zawadi za T-shirts zitatolewa kwaajili ya wanunuzi wa simu na vifaa aina ya Galaxy.
Kwa sasa nchini Tanzania kampuni ya Samsung ina maduka na vituo vya huduma kwa wateja katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam na ina mipango kabambe kuongeza huduma zake mikoa mingine.
Duka hili na kituo chake cha huduma kwa wateja vitatoa huduma siku za wiki yaani Jumatatu-Ijumaa kuanzia saa 9.30 asubuhi hadi 5.00jioni kwa Jumamosi ni kuanzia saa 9.30asubuhi hadi 1.00 mchana, litafungwa siku za Jumapili na Siku kuu.

 Kuhusu Vifaa vya kielektroniki vya Samsung
Teknolojia ya Samsung inatumiwa na watu takribani 236,000 katika nchi 79, inaleta mabadiliko na kuiwezesha dunia  kuingia kwenye teknolojia mpya na matumizi ya smart phone, luninga, air-conditioner, vifaa vya nyumbani vya kieletroniki, kamera, na vifaa vya maofisini kama kompyuta na printers ambavyo vina teknolojia ya hali ya juu kukidhi mahitaji ya wateja. Kujifunza mengi zaidi, tembelea www.samsung.com na www.facebook.com/SamsungMobileTanzania


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa