Arusha
Home » » WATUHUMIWA UGAIDI ARUSHA KIZIMBANI LEO

WATUHUMIWA UGAIDI ARUSHA KIZIMBANI LEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Watuhumiwa ugaidi Arusha kizimbani leoWATUHUMIWA 19 waliokamatwa na Jeshi la Polisi jijini Arusha wakihusishwa na matukio mbalimbali yanayoashiria ugaidi, ikiwemo milipuko ya mabomu na umwagiaji tindikali, wanatarajiwa kupanda kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi (ACP), Liberates Sabas, alisema jana kwamba kati ya watuhumiwa hao ni pamoja na Sheikh wa Msikiti Mkuu, Mustafa Kihago (46), na Imamu wake Abdul Azizi (49), ambao wote kwa kushirikiana na watu wengine wanatuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea nyumbani kwa Sheikh Abdul Jonjo na kumjeruhi katika eneo la Esso jijini hapa Oktoba 25, 2012.
Wengine wanaohusika na tuhuma hizo ni Yusuph Huta (30), na Kassimu Idrisa (34).
Kamanda Sabas, alitaja watuhumiwa wengine waliokamatwa na kuhusishwa na tukio la mlipuko wa bomu Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi eneo la Olasiti Mei 5, 2013 kuwa ni Huta, Ramadhani Waziri (28), Abdul Humu (30), Japhary Lema, Said Temba na Kassim Ramadhani (34). Wengine waliodaiwa kutekeleza unyama huo ni Abdulrahmani Hassan (41), mfanyakazi wa Benki ya Stanbic tawi la Arusha, Morris John Muha (44), Niganya Niganya (28), na Hassan Omar (40).
Aliwataja watuhumiwa wa tukio la mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa hitimisho la kampeni ya uchaguzi wa udiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kuua watu watatu na kujeruhi wengine kadhaa Juni 15, 2013 kuwa ni Huta (30), Humud (30), Lema (38), na Temba (42).
Pia, aliwataja watuhumiwa wengine walioongezeka baada ya mlipuko wa bomu katika mgahawa wa Vama kuwa ni pamoja na Kassim (34), Ramadhani (24), Abashar Omar (24), Abdulrahman Hassan (41), Morris (44), Niganya (28), Ntembo (40), na Hassan (40).
Akielezea tukio la kumwagiwa tindikali Sheikh Said Makamba wa msikiti wa Kwa Morombo Julai 11, 2013 aliwataja watuhumiwa watakaofikishwa mahakamani kuwa ni Huta (30), Ramadhan (28), Kassin Idrisa (34) na Lema (38).
Kamanda Sabas, aliwataja pia watuhimiwa waliodaiwa kuhusika na tukio la kumwagiwa tindikali Sheikh Kihago (49), kuwa ni pamoja na Huta (30,) Kassim (34), Lema (38), Hassan Mfinanga (57).
Aliwataja watuhumiwa wawili walioongezeka katika tukio la mlipuko wa bomu kwenye baa ya Arusha Night Park Aprili 13, 2014 kuwa ni Lema (38), na Ibrahimu Leonard (37), maarufu kama Sheikh Abuu Ismail (37).
 Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa