Arusha
Home » » ‘HATUUZI TENA MENO YA TEMBO’

‘HATUUZI TENA MENO YA TEMBO’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Serikali imefuta mpango wake wa kuuza shehena hazina ya meno ya tembo yenye thamani dola milioni 6o huku, ikipunguza vibali vya uwindaji wa Tembo nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu, akizungumza na mwananchi mara baada ya kuzindua utafiti wa sensa ya Tembo na Nyati katika eneo la Ikolojia ya hifadhi ya Serengeti na Masai Mara,alisema hata hivyo serikali haina mpango wa kutekeleza pembe hizo.
“ni kweli tuna hazina kubwa ya pembe katika bohari zetu zenye thamani ya dola 60 milioni lakini, kwa sasa tumesitisha mpango wa kuziana kama tulivyoomba awali”alisema.
Alisema wamesitisha kuuza ili kuzuia kuimarisha soko la kimataifa la meno ya Tembo.
Hata hivyo, mara mbili serikali ya Tanzania ilikwama kuuza hazina hiyo, kutokana na mashinikizo ya mashirika ya uhifadhi ya kimataifa ambayo yanazuia biashara ya meno hayo.
Akizungumzia sensa ya Tembo alisema licha ya kuongezeka kwa asilimia 266 kutoka mwaka 2006 hadi 2014, lakini wizara yake imepungiza kwa asilimia 50 vibali vya uwindaji Tembo.
“ingawa Tembo wanaongezeka lakini tunapunguza vibali vya uwindaji wa kitalii na hii itatuwezesha kuwa na idadi kamili ya tembo”alisema Nyarandu.
Alisema mpango huo, unakwenda sambamba na kufanya sensa ya Tembo wote nchini sambamba na wanyama wengine wakubwa,ikiwa ni sehemu ya mpango wa nchi za Afrika kupata idadi kamili ya Tembo.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa