Arusha
Home » » DIWANI CCM ARUSHA ATIMKIA CHADEMA

DIWANI CCM ARUSHA ATIMKIA CHADEMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) jijini Arusha kimepata pigo baada ya aliyewahi kuwa Diwani wake, Amos Mwanga kutimkia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mwanga alisema jana ameamua kujiunga na CHADEMA ili asaidie juhudi za kupambana na mafisadi waliopo serikalini wanaomaliza rasilimali za nchi kwa manufaa binafsi.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani hapa, Ephata Nanyaro alimkabidhi Mwanga kadi ya CHADEMA yenye namba 229791 na kurejesha kadi ya CCM namba 64141 iliyotolewa Juni 1988.
“CHADEMA imesaidia kupambana na ufisadi serikalini, nimeona niungane nao ili niongeze nguvu ya mapambano… hatuwezi kukaa tukidanganyana kila siku huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma muhimu,” alisema Mwanga.
Baada ya kumkabidhi kadi hiyo, Nanyaro alimkaribisha Mwanga kwenye uwanja wa mapambano ya kudai haki za wananchi huku akimwagia sifa kuwa ni kiongozi mahiri.
Mwanga alikuwa diwani wa Levelos kuanzia 2005 hadi 2010 aliposhindwa na mgombea wa CHADEMA, Nanyaro kwenye uchaguzi mkuu
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa