farm-chicken-412
Mwandishi Wetu Arusha
Zaidi ya wafugaji 300 wa Kuku na mifugo mbalimbali na wafanyabishara wa maduka ya madawa ya kilimo na mifugo wamepatiwa mafunzo ya utumiaji dawa mbalimbali za kutibu mifugo ya aina mbalimbali na virutubisho mbalimbali vinavyotolewa na kampuni ya BYTRADE (T) LTD ilikukwepa magonjwa ya mafuwa na aina nyingine za magonjwa na virutubisha vya mifugo.
Akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo wafugaji na wauza dawa za mifugo mkuu wa idara ya wanyama wa kampuni ya Bytrade Dkt Omary Magoma alisema kuwa aina mbalimbali za mifugo zimekuwa zikisumbuliwa na maradhi mbalimbali na zinahitaji dawa za kuyatibu maradhi yao ili kuweza kupata suluhu.
wafugaji+px
Magoma pia akawataka wafugaji pindi wanapoona wanyama wao wana hali dhaifu kuacha kuwapa dawa bila ya kugundua ugonjwa huku pia wakiendelea kuteketea na kuwashauri kutumia bidhaa za kampuni hiyo kwani ndio suluhu ya matatizo ya magonjwa na virutubisho ya wanyama na mimea.
“Kwa mfano dawa hii ya GUT-O-CID ni dawa ya kudhibiti kwa ufanisi bacteria waenezao magonjwa sumbufu kama salmonella,E.coli pia inadhibiti uzalishwaji wa gesi ya ammonia inayosababishwa harufu kali bandani ambayo ni chazo cha mafua makali kwa wanyama aina ya Kuku na Nguruwe”alisema Dkt Magoma.
Dawa hiyo ambayo huchanganywa kwenye chakula ukilinda chakula hicho dhidi ya maambukizi ya bacteria na fangasi na pia huongeza ladha ya chakula akabainisha kuwa kwa sasa wameingiza dawa aina kumi na moja sokoni na zinapatkana kwenye maduka mbalimbali ya  madawa ya mifugo humu nchini.
Dkt Magoma alizitaja baadhi ya dawa hizo kuwa ni suluhu ya maradhi yanayowaandama wanyama wafugwao kwa mfano dawa hii ya Mult-Aminovet ina aina zote za vitamin na amino acid pia madini kuweza kufidia mapungufu katika vyakula vya wanyama na kuboresha kiwango cha utagaji na ubora wa mayai.
Pia inaongeza matokeo bora kwa Ng’ombe wa maziwa na hutumika kuondoa stress wakati wa matibabu,chanjo,joto kali na usafirishaji kwa kuku huku pia akiitaja dawa aina ya Enziver kuwa inaboresha uyeyushwaji na unyonywaji wa chakula mwilini mwa wanyama na pia huraisisha ukuaji na ongezeko kubwa kwa Kuku na Nguruwe.
Huku akiwata watanzania hususani wafugaji kuanza kutumia dawa za kampuni hiyo kwani ndiyo suluhu ya kupata mifugo bora kwani dawa wanazouza zipo kwenye viwango vilivyo bora.