Arusha
Home » » MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZUNGUMZIA TUKIO LA BOMU KULIPUKA KWENYE BAA USIKU APRILI 13, 2014

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZUNGUMZIA TUKIO LA BOMU KULIPUKA KWENYE BAA USIKU APRILI 13, 2014

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu mbalimbali wakitazama mpira.
Blog hii imepata nafasi ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi
wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema
wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu
hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana alietekeleza shambulio hilo.
Kwenye maelezo mengine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.
Chanzo;Dj sek blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa