Arusha
Home » » Maofisa takwimu wapigwa msasa

Maofisa takwimu wapigwa msasa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAOFISA 50 kutoka idara za takwimu katika wizara, taasisi na vyuo vikuu vya serikali wanakutana jijini Arusha kupata mafunzo ya jinsi ya kuchambua takwimu za sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012 na kuoanisha na sera mbalimbali za nchi kama zinaendana.
Kukutana kwa maofisa hao kunafanyika siku 14 kabla rais
hajazindua kitabu cha tatu cha taarifa za takwimu zilizotokana na sensa hiyo.
Akizungumza na waandishi jana katika ufunguzi wa mafunzo hayo Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi, Hajati Amina Mrisho, alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa maofisa hao ili kuwawezesha kuandika taarifa za sensa kwa lugha rahisi zaidi zikiwa zimechambuliwa kwa kina.
“Haya mafunzo ya siku 10 yatahusisha makala 11 zilizoandaliwa kuhusu Elimu, Afya, Ajira, Vifo, Uzazi na Ndoa na hali ya umaskini katika nchi ili kusaidia kuoanisha na sera zilizopo kama zinaendana na takwimu zilizopatikana,” alisema Hajati Amina.
Akionyesha msisitizo katika hilo aliwataka wajumbe kushiriki katika mafunzo hayo kwa umakini na kasi ili itakapofika siku ya mwisho kila mmoja atoke na uwezo wa kwenda kuandaa takwimu katika idara yake na kuziandika kwenye kitabu kitakachotumiwa na idara husika kutengeneza sera na mikakati mbalimbali.
Alifafanua kuwa matokeo ya uchambuzi wa kina wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ni pamoja na kupata viashiria vitakavyowezesha Tanzania kutathmini na kufuatilia malengo ya Programu za Maendeleo ikiwemo dira ya maendeleo ya mwaka 2015 kwa Tanzania Bara na 2020 kwa Tanzania visiwani.
Awali akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliwasihi washiriki kuwa kipimo halisi cha mafanikio ya mafunzo hayo ni utoaji wa ripoti hizo kwa wakati na ubora unaotarajiwa.
“Dhamana ya mafanikio haya ipo mikononi mwenu  hivyo ni imani ya serikali kuwa mtatumia juhudi na maarifa ili lengo hilo litimizwe kikamilifu kwani wadau wanaotegemea taarifa hizo wanazisubiri ili wazitumie kupanga maendeleo,” alisema Mulongo.
Mafunzo hayo licha ya kufadhiliwa na mashirika ya kimataifa ikiwemo UNICEF pia yameshirikisha wakufunzi wataalamu kutoka US Bureau of Census na Havard University vya nchini Marekani kusaidia uboreshaji wa kuandika takwimu kwa lugha rahisi zaidi kutumiwa na 
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa