Arusha
Home » » Mafuriko yakosesha watu 872 makazi Arumeru

Mafuriko yakosesha watu 872 makazi Arumeru

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Moja ya nyumba ilibomoka baada ya mafuliko(Picha:Maktaba)
Wakazi 872  kutoka  kaya 72  za kata ya Bwawani iliyopo wilayani hapa hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mvua hizo ambazo zimesomba samani kwenye nyumba hizo na vyakula, pia zimeharibu mamia ya hekari za mazao ya aina mbalimbali  zilizokuwa zimepandwa na wakazi wa kata hiyo   katika vijiji vya Temi ya Simba na Bwawani .

Akizungumza na waandishi wa habari  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha , Fidelist Lumato alisema mvua hizo zilinyesha mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwaathiri zaidi watu waliokuwa wakiishi katika maeneo ya mabondeni

Lumato amewataka watu  wanaoishi katika maeneo ya mabonde kuhama ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Vilevile aliwataka kujenga nyumba imara kwa kutumia matofali ya kuchoma badala ya za matope ambazo zimekuwa zikisombwa na kubomoka mara kwa mara.

Kufuatia maafa hayo wadau mbali mbali  wamejitokeza kuwasaidia waathirika hao.  Halmashauri hiyo metoa msaada wa magunia 180 ya mahindi, mbegu  zenye thamani ya Sh. millioni 4.

Kampuni ya Monaban  kilo 2,000 za sembe ,Kampuni ya Tanform magodoro 50 na unga kilo 200, Msalaba Mwekundi,  Red Mross  mablanketi 100, ndoo 50 za kuchotea maji  na Kampuni ya A-Z vyandarua  250 na fulana  200 na Diwani wa Kata ya Mlangarini , Mathias Manga mabati 100 .
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa