Arusha
Home » » NEWS ALERT: MFANYABIASHARA WA MADINI ARUSHA AUAWA KWA KUPIGWA NA RISASI

NEWS ALERT: MFANYABIASHARA WA MADINI ARUSHA AUAWA KWA KUPIGWA NA RISASI

 
Mwili wa Erasto Msuya na mmiliki wa SG HOTEL mkoani Arusha mara baada ya kupigwa risasi zaidi ya sita na watu wasioj
ulikana na kufa papo hapo.
  Askari wakichunguza tukio la kupigwa kwa risasi kwa mfanya biashara huyu.
Mwili kulia mara baada ya kupigwa risasi na kulia ni gari la kifahari aina ya langer lover eneo linalodaiwa kupigwa risasi mfanyabiashara huyu. 

Habari zilizotufikia hivi punde Kutoka chumba chetu cha habari zinaeleza kuwa mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana kwa jina la Erasto Msuya na pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, amepigwa risasi zaidi ya sita na watu wasiojulikana na kufa papo hapo.

Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara. 

Habari zaidi tuvute subra kidoogo,tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.
Picha kwa hisani ya mdau Mutoto wa Arusha.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa