Arusha
Home » » Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa


 
 


Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa
Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha kwenye mkutano wa Chadema
Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni akiwa ndani ya gari ya jeshi baada ya kutiwa
nguvuni,





  Picha juu alipopiga picha na Viongozi mbalimbali wa Chadema
Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa
Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema,
Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada
ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika
Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni.
---
Yule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha Monduli
ametiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police.

Uchunguzi
wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama
alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari, ila aliwahi kuwa JKT na
akaacha. Amekuwa akivaa ngua hizo za jeshi kwa miaka mingi na wananchi
wa Mererani wanamtambua kama mwanajeshi.Kujua Habari zaidi jinsi mambo yalivyokua Bofya Hapa na BOFYA HAPA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa