Arusha
Home » » TUKIO ZIMA KATIKA PICHA BAADA YA ALIYE KUWA MBUNGE WA ARUSHA MJINI KUVULIWA UBUNGE,BAADHI YA WAFUASI WAPOTEZA FAHAMU.

TUKIO ZIMA KATIKA PICHA BAADA YA ALIYE KUWA MBUNGE WA ARUSHA MJINI KUVULIWA UBUNGE,BAADHI YA WAFUASI WAPOTEZA FAHAMU.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (katikati), akiwa amekaa na Mbunge Mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (kushoto), akimpa moyo, baada ya hukumu kutolewa.
Mmoja wa wafuasi wa Chadema, Naomi Solomon (56), akiwa amepoteza fahamu, mara baada ya mahakama kutangaza kumtengua Ubunge Godbless Lema.

Makada watatu waliofungua kesi dhidi ya Lema, Agnes Mollel…


Mmoja wa wafuasi wa Chadema, Naomi Solomon (56), akiwa amepoteza fahamu, mara baada ya mahakama kutangaza kumtengua Ubunge Godbless Lema.
Makada watatu waliofungua kesi dhidi ya Lema, Agnes Mollel (kulia), Happy Kivuyo (mwenye koti jekundu) na mwisho Musa Mkanga, wakifurahi mahakamani mara baada ya hukumu kutolewa.

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katikati  akihutubia umati wa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamefurika mahakamani  kusikiliza shauri la kupinga ubunge wake, ambapo mahakama imeutengua ikidai Lema alikiuka sheria za uchaguzi na kuamuru uchaguzi urudiwe.
Askari polisi wakiwa eneo la mahakama wakiimarisha ulinzi muda mfupi baada ya mahakama kutengua ubunge wa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutoka Chadema.

Lema akiwatia moyo wafuasi wa chadema katika eneo la mahakama baada ya kupokea matokeo ya kutengua ubunge wake leo, huku akieleza kuwa hata kata rufaa ila anasubiri tume ya uchaguzi itangaze rasmi kuanza kwa uchaguzi katika jimbo la Arusha Mjini.

Polisi wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Umati wa wafuasi wa Chadema ukisikitishwa na uamuzi wa mahakama ya mjini Arusha, ulitolewa na Jaji, Gabriel Rwakibarila wa mahakama kuu kanda ya Sumbawanga.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa